Moto wateketeza mabweni mawili, vitanda 73 Ashira Sekondari

0
814

Safina Sarwatt-Moshi,

Mabweni wa mawili ya shule ya sekondari ya wasichana ya Ashira iliyopo Marangu wilayani Moshi, mkoani Kilimanjaro yameteketea kwa mtoto na kusababisha hasara ya vitanda 73 pamoja na vifaa vya wanafunzi.

Mkuu wa wilaya Moshi Kippi Warioba amesema kwa kamati ya ulinzi na usalama wilaya imechukua hatua na kwamba wanaendelea kuchunguza chanzo cha mtoto huo ambao umezuka saa moja na nusu asubuhi  wakati wanafunzi wakijandaa kungia darasani.

“Moto umesababisha hasara kubwa ya magodoro 73, vitanda 73, madaftari ya wanafunzi na nguo na kamati ya ulinzi na usalama imeanza taratibu ili kuwaweka wanafunzi katika mazingira ya usalama,”amesema.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wameiomba serikali kuimarisha hali ya ulinzi na usalama wa wanafunzi ambao wamepoteza mali zao.

“Tulikuwa tunajiandaa kuingia darasani gafla tunaitwa na mkuu wa shule kwamba mabweni yanawaka moto lakini hatukuweza kuokoa vitu vyetu vyote vimeteketea kwa moto na tumebaki na sare za shule tuliyovaa mwilini,” amesema mmoja wa wanafunzi, Naima Akida.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here