29.3 C
Dar es Salaam
Friday, September 20, 2024

Contact us: [email protected]

Wizara inakamilisha kanuni za uuzaji nyamapori kwenye mabucha maaluma

Ramadhan Hassan,Dodoma

Wizara ya Maliasili na Utalii imesema inakamilisha kanuni za uwindaji ambazo zitaruhusu uanzishwaji wa vituo na taratibu za kuuza wanyamapori kwenye mabucha maalum.

Hayo yameelezwa leo bungeni Mei 23 na Waziri wa Wizara hiyo,Dk.Hamisi Kigwangala wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yake kwa mwaka 2019-2020.

Waziri Kigwangala amesema kuwa wizara inakamilisha kanuni za uwindaji wenyeji ambazo zitaruhusu uanzishwaji wa vituo na taratibu za kuuza Wanyamapori kwenye mabucha maalum.

Waziri Kigwangala amesema Serikali imepiga hatua katika kutokomeza ujangili ambapo matokeo ya sensa ya tembo katika mfumo wa ikolojia wa Selous-Mikumi iliyofanyika mwaka jana, inaonyesha idadi ya tembo haipungui.

Dk.Kigwangala amesema katika sensa hiyo haikubainika mizoga mipya ya tembo waliouawa na majangili katika mfumo huo wa ikolojia.

“Sote tunashuhudia kuongezeka idadi ya tembo na wanyamapori wengine waliokuwa wakiwindwa na majangili. Hali hiyo inasababisha wanyamapori kuanza kuonekana katika maeneo ambayo awali haikuwa rahisi kuwaona. Mfano hivi karibuni tembo wameonekana eneo la Chuo Kikuu Cha Dodoma mara mbili,” amesema.

Amesema Serikali imekuwa ikitumia mbinu mbalimbali kupambana na ujangili ambazo ni kutumia ndege zisizokuwa na rubani,pilipili na mizinga ya nyuki.

“Mbinu zingine zinazotumika ni ndege zisizokuwa na rubani, pilipili, mizinga ya nyuki, matumizi ya vifaa vinavyopiga kelele na mwanga mkali, kuweka minara ya kuangalia mbali katika maeneo yanayokabiliwa na changamoto pamoja na kutoa elimu kwawananchi kuhusu tahadhari na mbinu za kuepuka madhara ya wanyamapori.
“Katika kukabiliana na changamoto ya mamba na viboko, sensa ya wanyamapori inaendelea katika maeneo ya Ziwa Rukwa na mito inayopita vijijini na nje ya hifadhi,”amesema.

Dk. Kigwangala amesema matokeo ya sensa hiyo yataonyesha idadi ya mamba wanaopaswa kupunguza katika maeneo yenye matukio ya wananchi kujeruhiwa na kuuawa na mamba.
Alibainisha kuwa wizara imeendelea kulipa kifuta jasho na machozi kwa wananchi kufuatia uharibifu wa mali a upotevu wa maisha uliotkana na wanyamapori wakari na waharibifu.
“Hadi Machi mwaka huu, sh. bilioni 1.4 zimelipwa kwa wananchi 7,320 na wilaya 57 ama kifuta jasho na machozi,amesema Dk. Kigwangala

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles