Arodia Peter, Dodoma
Mkoa wa Kagera upo mbioni kujengwa kituo maalum cha kuuzia kahawa eneo la Nyakanazi ili wakulima waweze kunufaika na kilimo hicho.
Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Halima Bulembo(CCM), bungeni leo Mei 14, Naibu Waziri wa Fedha, Dk. Ashatu Kijaji amesema Mkoa wa Kagera ni pekee unaopakana na nchi za Afrika Mashariki ( EAC) kwa hiyo kituo hicho kitakuwa na fursa pekee kwa mkoa huo kunufaika na jiografia hiyo.
Katika swali lake la msingi, Halima alitaka kujua Serikali ina mpango gani wa kuifanya Kagera ifaidike na uchumi wa jiografia yake, ikizingatiwa kuwa mkoa huo unaongoza kwa kulima kahawa aina ya robusta nchini.