29.7 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Sweden yafungua upya kesi ya ubakaji dhidi ya Assange

STOCKHOLM, SWEDEN

WAENDESHA mashitaka wanafungua upya kesi ya ubakaji dhidi ya muasisi wa tovuti ya uvujishaji wa nyaraka za siri (Wikileaks), Julian Assange.

Hilo limerahisishwa baada ya Assange kuondolewa kutoka ubalozi wa Ecuador mjini London, Uingereza mwezi uliopita, ambako alikuwa amepewa hifadhi ya ukimbizi.

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Mwendesha Mashitaka nchini Sweden, Eva-Marie amewaambia wanahabari mjini hapa kuwa kuna sababu za kutosha kushuku kuwa Assange alifanya kitendo cha ubakaji.

Awali waendesha mashitaka hao walifungua dhidi ya Assange alipoitembelea nchi hiyo mwaka wa 2010.

Miaka saba baadaye, kesi ya madai ya ubakaji ikafutwa baada ya muda wa kuiendesha kesi hiyo kumalizika.

Hata hivyo, mtandao wa Wikileaks umesema kufunguliwa kwa kesi hiyo dhidi ya Assange kutampa nafasi ya kulisafisha jina lake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles