25.6 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

DC Mjema: Mama yangu alinilea kwa shida

MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

MKUU wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amesema kuwa Siku ya Mama Duniani ni maalumu inayotoa nafasi ya pekee ya kutoa shukrani kwa mama.

Akizungumza juzi jijini hapa wakati wa maadhimisho hayo yaliyokuwa na kaulimbiu ya ‘MamaYangu, Shujaa wangu, Nyota Yangu’, Mjema alisema kuwa mama yake aliweza kumlea kwa shida lakini sasa anafurahia matunda yake.

 “Mama yangu ni shujaa kwa malezi aliyonipatia pamoja na kipato chake kutokidhi mahitaji yoyote.

“Aliweza kunilea kwa shida lakini leo nafurahi na kuona matunda yake. Kwa hivyo siku ya leo mama yangu ndio shujaa wangu 2019, mama yangu, nyota yangu.

“Hii siku maalumu kwa sisi wote kuungana pamoja na kuweza kuwapa ushujaa wa kipekee mama zetu. Ni imani yangu kuwa hapa kila mmoja anayo stori ambayo inamfanya mama kuwa shujaa wake leo.

“Nawashukuru sana waandaaji wa maadhimisho haya kwani imekuwa ni siku muhimu lakini ilikuwa haipewi umuhimu wake kama inavyostahili.

“Nawaomba wote tuweke kwa vitendo ushujaa wa mama zetu lakini sio kwa maneno tu,” alisema Mjema.

Katika kusherehekea siku hiyo ambayo huadhimishwa Mei 12 ya kila mwaka, waandaaji Kampuni ya Fern Tanzania Ltd kwa kushirikiana na wadau mbalimbali walitoa tuzo mbalimbali kwa watu walioandika historia ya jinsi ya kuwakumbuka mama zao kutokana na kazi nzuri waliyoifanya kwa malezi hadi kufikia sasa.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo,  Liginiku Millinga, alisema kuwa kampuni yake iliungana na wadau wengine ili kuweza kufanikisha siku hiyo.

“Sisi tuliona kuna umuhimu wa kusherehekea siku hii na ndiyo tukaona umuhimu wa kushirikisha wadau wetu ambao kila siku huwa tunafanya kazi nao ili kuweza kuifanya Siku ya Mama Duniani kuwa ya kipekee kwa mwaka 2019,” alisema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles