23.9 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Kuyumba kwa ndoa huaribu watoto kisaikolojia – Waziri

KHAMIS SHARIF -ZANZIBAR

NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Simai Muhamed Said, amesema ndoa zinazoyumba na zenye mizozo husababisha watoto kuathirika kisaikolojia katika maisha yao.


Hayo aliyasema jana kisiwani Unguja alipokuwa akizungumza na wahitimu wa mafunzo ya maadili ya ndoa kwa wanandoa na wanaotarajiwa kufunga ndoa hivi karibuni.


Simai alisema kuwa ndoa nyingi ambazo ufanyika kwa gharama kubwa ndizo zimekuwa zikikosa maisha na kusababisha ongezeko la talaka.
Alisema ndoa hizo zimekuwa zikivunjika katika kipindi kifupi na kusababisha familia ya mume na mke kubaki katika simanzi na huzuni kubwa.


“Subira, uvumilivu na mapenzi ya kweli ni mambo yaliyokosekana katika ndoa za siku hizi na kusababisha kuvunjika.
“Tukiimarisha ndoa kwa masilahi ya kizazi, hakika tutakuwa tumefuata maadili ya dini, sasa tutoke hapa tujue ni wahitimu na walimu wazuri.
“Mafunzo haya yatoshe kabisa kubadilisha ndoa zetu na kuwa bora kwa kuizima migogoro na mizozo ya ndoa katika nyumba zetu,” alisema.


Aliwataka wahitimu wa mafunzo hayo kuimarisha ndoa zao kwa masilahi ya vizazi vyao na kuwa walimu kwa jamii katika kutoa elimu waliyoipata.
Naye Katibu wa Ofisi ya Mufti Mkuu Zanzibar, Sheikh Fadhil Suleiman Soraga, alisema Serikali kupitia Ofisi ya Mufti imeamua kutoa mafunzo hayo kutokana na ongezeko kubwa la talaka, na kuwataka wahitimu hao vyeti walivyopatiwa visiwe ni pambo bali kuyafanyia kazi kwa vitendo mafunzo hayo.


Awali akisoma risala, mmoja wa wahitimu hao, Khadija Mussa, aliiomba Serikali kupitia Ofisi ya Mufti iweke cheti cha mafunzo ya ndoa kuwa kipengele cha kuzingatia kama ilivyo cheti cha kupima Ukimwi ambacho ni muhimu kwa wanaotaka kufunga ndoa.


Jumla ya wahitumu 43 wametunikiwa vyeti baada ya kumaliza mafunzo hayo wakiwemo wanawake 26 na wanaume 17.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles