28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Polisi hawatowi fedha kununua chakula cha mahabusu- Waziri

NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Hamadi Masauni amesema  hakuna utaratibu wa askari polisi kutoa fedha zao mfukoni kwa ajili ya chakula cha mahabusu.

Kauli hiyo aliitoa jana bungeni alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Masasi, Rashid Chuachua (CCM).

Katika swali lake Mbunge huyo alitaka kujua serikali ni lini itarekebisha utaratibu uliopo ambapo askari wanalazimika kutoa pesa zao mfukoni ili kuwapa chakuka mahabusu.

Masauni alisema utaratibu uliopo  ni kwa serikali kupitia Jeshi la Polisi ina wajaibu wa kuwapatia chakula mahabusu waliopo kororkoroni.

“Ndugu wa Mahabusu pia wanaruhusiwa kupeleka chakula kwa mahabusu wao ambao wapo korokoroni,” alisema Masauni .

Alisema serikali inatambua uhaba wa vitendea kazi kwa Jeshi la Polisi ikiwa ni pamoja uchache wa  magari na nyumba za askari.

Alisema kwa sasa Wilaya ya Masasi ina nyumba za makazi ya askari zipatazo 15 ambazo zinzishi familia 30.

Alisema ni kweli askari wengine 154 bado wanaishi uraiani lakini hata hivyo serikali itaendelea kujenga nyumba za makazi ya askari kwa awamu kwa kadri upatikanaji wa fedha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles