27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali ina mfumo wa kutatua migogoro

OFISI  ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imesema serikali ina mfumo wa kisheria wa kutatua migogoro kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Hayo yalielezwa jana bungeni na Naibu Waziri wa Wizara hiyo,Mwita Waitara alipokuwa akijibu swali la  Mbunge wa Viti Maalum Yosepher Komba (Chadema).

Katika swali lake Yosepher alitaka kujua ni lini serikali itawawekea wananchi wanasheria ili kusaidia kutatua migogoro ya ardhi.

Waitara alisema mfumo huo umeainishwa katika utatuzi wa migogoro ya ardhi namba 2 ya mwaka 2002 na kanuni zake.

Alisema migogoro ya ardhi iliyopo Wilayani Muheza imegawanyika katika makundi matatu ambayo ni migogoro ya kiwilaya, ambayo inahusisha mipaka ya Vijiji vya Wilaya ya Muheza na Tanga jiji pamoja na Vijiji vya Muheza na Pangani.

“Migogoro hiyo inashughulikiwa katika ngazi ya Mkoa na itapatiwa ufumbuzi wakati wowote,” alisema.

Alisema kundi la pili la migogoro ni ile ya mipaka ya vijiji iliyotokana naa zoezi la upimaji wa mipaka nchi nzima uliofanyika mwaka 2007.

Naibu huyo alilieleza bunge kuwa migogoro mingine ni migogoro ya viwanja ambayo hupokelewa na kutatuliwa kwa utaratibu wa kawaida wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa.

Alisema suluhisho la kudumu kwa aina  hiyo ya migogoro ni kukamilisha mpango wa matumizi bora ya ardhi kupima viwanja  

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles