Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Katibu wa Chuo cha Ulinzi (NDC), Kanali Furahisha Ntahena, amesema zoezi la upandaji miti lililozinduliwa leo lina lengo la kuimarisha utunzaji wa mazingira katika maeneo ya jeshi.
Jenerali Ntahena ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Aprili 5, baada ya kumaliza zoezi kupanda miti 2,000 lililofanywa na viongozi na wanafunzi wa kundi la saba la chuo hicho pamoja na watendaji wa Wakala wa Misitu nchini (TFS) lililofanyika katika Mto Tegeta uliopo karibu na chuo hicho.
Amesema shughuli ya upandaji miti katika eneo hilo linafanyika baada ya kupokea ushauri kutoka kwa watalaamu ambao waliwatahadharisha kuhusu uharibifu wa mazingira uliofanyika katika maeneo yanayozunguma jeshi.
“Tuliona tutumie nafasi ya washiriki wanafunzi wa chuo hichi ambao wanashiriki kozi,wao TFS walitushauri tukakagua mazingira yetu kazi tukaona jinsi yalivyoathirika na kwakuwa wana mamlaka wakaleta miti ili tuje kupandai.
“Zoezi hili ni endelevu kwa makambini na majumbani kila mwanajeshi kila mtumishi wa maliasili na vyombo vya ulinzi na usalama tuna mpango wa kuwapatia miti kulingana wanavyohitaji wakapambe na tutaikagua,” amesema Kanalu Ntahena.
Aidha, amesema wananchi wanapaswa kushirikiana katika kutunza mazingira na hawajafikiria kukata mti mmoja wanapaswa kuwaza umetumia miaka mingapi kukua.
Kwa upande wa Meneja wa Misitu Wilaya ya Kinondoni kutoka TFS, Dotto Ndumbikwa, amesema wakala wanatoa wito kwa wananchi kutunza mazingira kwa kuwapa miche wananchi, taasisi na mashirika ili waweze kupanda na kuacha kukata miti ovyo na kuacha kuchimba mchango.
Amesema miti iliyopandwa leo ni pamoja na miti ya mbao, mifenesi, rusina na cinderela.