Na PATRICIA KIMELEMETA – Dar es Salaam
MAMLAKA ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) imebaini uwepo wa pipi hatari ambazo zinadaiwa kuchanganywa na dawa za kulevya na kusambazwa shuleni kuwauzia wanafunzi.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Kamishna Mkuu wa mamlaka hiyo, Rogers Sianga alisema kuna pipi zilizochanganywa na dawa za kulevya ambazo zinauzwa katika maeneo ya shule mbalimbali kuanzia zile za awali hadi sekondari.
Baada ya maelezo mafupi ya Sianga, ofisa wa mamlaka hiyo ambaye anashughulika na uchunguzi wa dawa hizo katika maeneo ya shule mbalimbali, alisema pipi hizo zinauzwa kati ya Sh 100 na 200.
Ofisa huyo ambaye jina lake tunalihifadhi kwa sababu za kiusalama, alisema watumiaji wakubwa wa pipi hizo ni wanafunzi kuanzia …
Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.