25.7 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

Magufuli aagiza taasis zote za kifedha ziunganishwe

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam

Rais Dk John Magufuli ameigiza Wizara ya Fedha na Mpango kuunganisha taasis za kifedha ziwe chini ya mfumo mmoja wa kimawasiliano utakaoirahishia Serikali kujua mapato yanayokusanywa lakini pia kupunguza gharama za uendeshaji wa kila taasis.

Ametoa agizo hilo leo Ijumaa Januari 18, alipokuwa akihutubia viongozi mbalimbali na wananchi waliojitokeza katika Makabidhiano ya mfumo wa usimamizi wa mawasiliano ya simu (TTMS) nchini, uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli amesema mfumo huo utarahisisha taasis hizo hasa ya ukusanyaji mapato kwani taarifa zitakuwa za uwazi hivyo itapunguza udanganyifu na ubadhirifu wa fedha unaofanywa na baadhi ya watumishi wasio wazalendo.

“Naiagiza Wizara ya Fedha kuhakikisha taasisi zote za kukusanya mapato na za kifedha ziunganishwe na mfumo mmoja wa kieletroniki utakaowasaidia kufanya kazi zao kisasa zaidi.

“Nitashangaa kama hazitaungaishwa mtafanya niamini mnafanya kazi gizani na mimi nataka tuwe na tochi ya kuwamulika na tochi hiyo ni kuwa na mfumo unganishi,” amesema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli amesema bila mfumo huo serikali ingeendelea kupoteza fedha nyingi bila kujua kwani wanaotakiwa watote taarifa za ukusanyaji mapato wangeleta kile wanachokitaka wao bila mtu mwingine kujua lakini sasa taarifa zote zitakuwa wazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles