28.3 C
Dar es Salaam
Friday, October 4, 2024

Contact us: [email protected]

Homa ya mapafu ugonjwa hatari unaochangia vifo vingi nchini

Ramadhan Hassan, Dodoma

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto, imeyataja magonjwa 10 yaliyochangia vifo vya watu 20,087 mwaka 2018, huku homa ya mapafu ikiongoza na shinikizo la damu ikiingia kwa mara ya kwanza katika orodha hiyo.

Waziri wa wizara hiyo, Ummy Mwalimu amesema hayo leo Ijumaa Januari 18, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya huduma ya afya nchini katika kipindi cha mwaka 2018.

Amesema takwimu zilizokusanywa kupitia mfumo wa DHIS2 zimeanisha kuwa mwaka 2018 kumetokea jumla ya vifo 20,087 ikilinganishwa na vifo 19,693 mwaka 2017 vilivyosababishwa na magonjwa hayo 10.

Ameyataja magonjwa mengine na idadi ya watu iliyoua katika mabano kuwa ni  ugonjwa wa moyo (1,253), malaria (693) sawa na asilimia 3.4, Ukimwi (605) sawa na asilimia tatu, kifo cha mtoto tumboni (ngozi haijachubuka) (540), sawa na asilimia 2.7, magonjwa mengine (538) sawa na asilimia 2.7.

Mengine ni maambukizi katika damu (496) sawa na asilimia 2.5 na shinikizo la damu (382) sawa na asilimia 1.9.

“Katika kipindi cha miaka miwili (2017 na 2018) homa ya mapafu imeongoza kwa kusababisha vifo vingi ambapo 2017 ilichangia asilimia 18.2 ya vifo vyote na mwaka 2018 ugonjwa huo umesababisha vifo kwa watu 2,590 ambapo umechangia kwa asilimia 12.9 ya vifo vyote,” amesema.

Aidha, amesema mwaka 2018 ugonjwa usio wa kuambukiza wa shinikizo la damu umejitokeza katika magonjwa 10 yanayoongoza kwa kusababisha vifo ambapo umechangia vifo kwa asilimia 1.9 ya vifo vyote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles