23.3 C
Dar es Salaam
Sunday, October 6, 2024

Contact us: [email protected]

Kindoki kutomzika baba yake

Lulu Ringo, Dar es salaam.

Licha ya kufiwa na baba yake, mlinda mlango wa Klabu ya Yanga, Klaus Kindoki hataweza kumzika mzazi wake huyo aliyefariki dunia leo nchini Congo, kwani atakuwa mmoja wa wachezaji watakaotumika katika mchezo wa kesho dhidi ya Stand United.

Baba yake Kindoki anatarajiwa kuzikwa Jumapili hii Januari 20, huko huko nchini Congo.

Akizungumza na Mtanzania Digital, Mratibu wa timu hiyo Hafidh Salehe, amesema mchezaji huyo atashindwa kushiriki katika mazishi ya baba yake kutokana na kutegemewa na klabu katika michezo mbalimbali.

“Kindoki hatasafiri maana tunamtegemea katika mchezo wa kesho na michezo mingine, hatuna golikipa mwingine atakayeweza kuchukua nafasi yake kwa sababu mbadala wake Ramadhani Kabwili ni mgonjwa,” amesema Hafidh.

Yanga iko mkoani Shinyanga kuvaana na Stand United katika mchezo wa duru ya pili ya Ligi Kuu Tanzania Bara, mchezo utakaopigwa kesho Januari 19, saa 10 jioni katika dimba la Kambarage mkoani humo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles