33.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yawataka Ma-DC wasitoe leseni za misitu kwa muda usiojulikana

Hadija Omary, Lindi

Serikali Mkoani Lindi imewataka wakuu wa wilaya mkoani humo kutogawa leseni mpya za uvunaji wa misitu kwa muda usiojulikana.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa huo, Godfrey Zambi jana alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari.

Zambi amesema amelazimika kutoa zuio hilo kutokana na kuwepo kwa uvunaji holela wa misitu unaoendelea kwa sasa  pamoja na kutumika kwa leseni zilizokwisha muda wake kunakosababisha kuwepo na biashara za magendo mkoani humo.

“Najua TFS (Wakala wa Misitu) ni taasisi ya serikali na mimi kama msimamizi wa serikali na msimamizi mkuu wa misitu katika mkoa huu, nawaagiza wakuu wa wilaya wote kutotoa leseni mpya tena hadi tutakapowatafakari upya watu hawa tuliowapa dhamana,” amesema Zambi.

Zambi amesema kutokana na doria mbalimbali alizozifanya katika siku za hivi karibuni amegundua kuwepo kwa uharibifu wa misitu na endapo  isiposimamiwa vizuri  kuna hatari kubwa kwa misitu hiyo kupotea.

Pamoja na mambo mengine, Zambi amesema katika kufanya marekebisho ya jambo hilo atafanya mawasiliano na Mkurugenzi wa TFS ili wakae pamoja na kukubaliana utaratibu mpya wa namna  ya kusimamia rasilimali za misitu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles