26.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

Zitto ahofia usalama wake

ANDREW MSECHU-DAR ES SALAAM

KIONGOZI wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema anahofia usalama wake kutokana na taarifa alizozipata, akisema kuna mpango wa kumdhuru.

Kiongozi huyo wa upinzani ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kusimamia agenda za muungano wa vyama 10 vya upinzani kuanzia mwishoni mwa mwaka jana, alieleza kupitia mtandao wa Twitter, akionya wale walionuia kumdhuru.

Katika ukurasa wake wa Twitter, Zitto Kabwe ameandika: “Tunafahamu kuwa Operesheni Maalumu #Mzizima2 imepewa kibali kutekelezwa. Dhima ‘ Vita ya Mwisho kuleta Nidhamu kamili’ inataka kinachoitwa kumnyamazisha SAI( mie huyo). Wakajipange upya Tu. Mungu tu Ndio anaweza kuninyamazisha. SIOGOPI mwanadamu mwenzangu aslani” alisema katika ukurasa huo.

MTANZANIA ilipomtafuta kwa ajili ya kupata ufafanuzi wa suala hilo, Zitto alisema amepata taarifa hizo kutoka kwa vyanzo vyake lakini hawezi kutoa taarifa  kwa kina.

“Suala la usalama ni suala nyeti sana, kwa hiyo habari nilizotoa ndiyo hizo hizo. Kukiwa na jingine nitaeleza. Ile Tweet inatosha, ndiyo maelekezo niliyopewa na walionipa taarifa. Siwezi kwenda mbali zaidi maana naweza kujikuta nawaharibia maisha walionipa taarifa,” alisema.

Alipoulizwa iwapo amewasilisha au kutoa rasmi taarifa hizo polisi kwa ajili ya kulipa jeshi hilo jukumu la kufuatilia suala hilo, akisema. “Sijatoa taarifa Polisi kwa sababu maalumu” alisema.

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alipoulizwa kuhusu taarifa hizo, alisema Zitto anatakiwa kutoa taarifa rasmi katika kituo chochote cha polisi ili waanze kuchukua hatua.

Alisema suala hilo linahusu usalama wake na halitakiwi kuishia kuripotiwa kwenye mitandao ya kijamii kwa kuwa jeshi hilo haliwezi kuanza kufuatilia kwenye mitandao hiyo kwa aajili yakuchukua hatua.

“Wakati mwingine, hayo mambo wanayafanya kwa sababu zao za kisiasa, kama hawezi kuripoti polisi hilo linaweza kuchukuliwa kuwa ni siasa tu…,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles