25.3 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Makamu Mkuu UDOM afariki dunia, JPM amlilia

MWANDISHI WETU

RAIS Dk. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Benjamin  Mkapa kutokana na kifo cha  Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Egid Beatus Mubofu kilichotokea jana   Pretoria, Afrika Kusini.

Profesa Mubofu alipelekwa   Pretoria kwa matibabu zaidi akitokea Taasisi ya Tiba ya Mifupa ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MOI) alikokuwa akipatiwa matibabu ya kiharusi.

Mkurugenzi wa Mawailiano Ikulu, Gerson Msigwa alisema Rais Magufuli amemuomba Mkapa kufikisha salamu zake za pole kwa familia ya marehemu Profesa Mubofu, wahadhiri na wafanyakazi, wanafunzi wote wa UDOM, jumuiya na taasisi zote ambazo Profesa Mubofu alifanya kazi na wote walioguswa na msiba huo.

“Nimesikitishwa  nakifo cha Profesa  Mubofu, nitamkumbuka kwa uchapakazi wake, ubunifu, uadilifu na uaminifu mkubwa aliouonyesha katika utumishi wake kwa taifa ikiwamo kazi nzuri aliyoifanya katika Shirika la Viwango la Taifa (TBS) akiwa Mkurugenzi Mkuu kabla ya kuteuliwa kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha UDOM,ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Rais Magufuli ameiombea familia ya marehemu Profesa  Mubofu kuwa na moyo wa subira na uvumilivu na amemuombea kwa Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yake mahali pema peponi. Amina.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles