27.8 C
Dar es Salaam
Monday, December 6, 2021

Wanakwaya wawili wafia kanisani

PASCHAL MALULU – KAHAMA

WAUMINI wa Kanisala Waadventista Wasabato (SDA) wakazi wa Mtaa wa Igomelo Wilaya ya Kahama, wamefariki dunia baada ya kuangukiwa na ukuta ndani ya kanisa hilo na wengine 10 wakijeruhi.

Ukuta huo ulianguka baada ya mvua kubwa ya mawe na upepo mkali kuangusha ukuta na kuwaponda waumini hao  wakiwa kwenye mazoezi ya kwaya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Simon Haule alisema tukio hilo lilitokea saa 10 jioni baada ya mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha.

Aliwataja waliofariki dunia kuwa ni Juneth Edward (35) na Elisha Masai (5) wote wakiwa wakazi wa Mtaa wa Igomelo wilayani Kahama.

Kamanda Haule aliwataja waliojeruhiwa katika tukio hilo ni kuwa ni Eva Simon (30), mwalimu wa Shule ya Msingi Korogwe, Upendo Daniel (25) mkazi wa Mtaa wa Malunga, Ayubu Kisunda (37) mkazi wa Masaki, Mary Maduhu (35) mkazi wa Masaki, wote  Wilaya ya Kahama.

Wengine ni Stephen Shija (23) mkazi wa Kakola Msalala, Paul Ibrahim (25) mkazi wa Igomelo, JaclinJohn (25) mkazi wa Masaki, Irene Danel (5), Rahel Emanuel (30) mkazi wa Masakina Mariam Kishegena (30) mkazi wa Igomelo.

Kamanda Haule alisema miili ya marehemu imehifadhiwa Hospitali ya Wilaya ya Kahama kwa uchunguzi wa madaktari huku majeruhi wakiendelea na matibabu hospitalini hapo.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,340FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles