25.3 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Mtoto wa Ronaldo atwaa tuzo Italia

TURIN, ITALIA

MTOTO wa Cristiano Ronaldo, Cristiano Jr, ameanza kufuata nyayo za baba yake baada ya kutwaa tuzo kutokana na mchango wake kwenye kikosi cha Juventus cha vijana chini ya miaka tisa.

Ronaldo raia wa nchini Ureno ambaye anakipiga katika klabu hiyo ya Juventus, alitumia ukurasa wake wa Instagram na kuposti picha ya mwanawe akiwa na tuzo hiyo kisha kuandika ‘Parabens’ akimaanisha hongera.

Cristiano Jr, anaitumikia timu hiyo ya vijana mara baada ya baba yake kujiunga akitokea Real Madrid kwa uhamisho wa pauni milioni 100.

Septemba mwaka huu kijana huyo mwenye umri wa miaka nane, aliifungia timu yake mabao manne katika mchezo dhidi ya Lucento, hivyo amepewa tuzo hiyo kutokana na mchango wake mkubwa ndani ya timu.

Hata hivyo, Ronaldo anaamini mtoto wake atakuja kuwa mchezaji bora duniani kama alivyo yeye kwa sasa kutokana na vile anavyomwandaa.

“Ninaamini mwanangu atakuja kuwa staa hapo baadaye, hata miminilianza hivyo wakati nina umri mdogo, nina asilimia 100 atakuja kuwa bora duniani,” alisema Ronaldo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles