BRUISSELS, UBELGIJI
MAHAKAMA ya Sheria ya Ulaya (ECJ) jana imetoa uamuzi kuwa Serikali ya Uingereza inaweza kuubatilisha uamuzi wake wa kujiondoa umojani humo (Brexit) bila ya kutafuta ridhaa ya nchi nyingine wanachama.
Uamuzi huo umetolewa siku moja kabla ya wabunge waUingereza hawajapiga kura kuamua kama wayaunge mkono makubaliano ya Brexit yaliyofikiwa kati ya Uingereza na Umoja wa Ulaya au la.
 Uamuzi wa ECJ unaoenekana kama ushindi kwa watu wanaotaka kura nyingine ya maoni ifanyike Uingereza itakayoizuia nchi hiyo kuondoka EU mwakani.
Waziri wa Mazingira wa Uingereza, Michael Gove amesema mpango wa Waziri Mkuu Theresa May utapigiwa kura hiyo leo, kama ilivyopangwa.
Hata hivyo, taarifa zilizojitokeza baadaye jioni zinaonesha kuwa huenda mchakato huo wa kura bungeni unaweza usiwepo leo hadi itakapotangazwa tena.