26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 14, 2024

Contact us: [email protected]

‘Siwezi kupumua’, yalikuwa maneno ya mwisho ya Khashoggi

WASHINGTON, MAREKANI

KITUO cha Televisheni cha CNN nchini Marekani kimesema maneno ya mwisho yaliyotamkwa na mwandishi habari wa Saudi Arabia, Jamal Khashoggi yalikuwa ‘siwezi kupumua’.

CNN imezinukuu duru za mtu aliyesoma mkanda wa sauti iliyorekodiwa dakika za mwisho kabla ya mauaji ya Khashoggi.

Duru hizo zimeiambia CNN kwamba nakala hiyo inaonesha wazi mauji ya Khashoggi yalipangwa kabla na simu kadhaa zilipigwa ili kutoa maelezo mafupi kuhusu mchakato huo.

CNN imesema maafisa wa Uturuki wanaamini simu hizo zilipigwa na maafisa wa ngazi za juu wa Saudia.

Mkanda huo unaonesha kulikuwa na mapambano na mtu anayeaminika kuwa Maher Abdulaziz Mutreb, mwadiplomasia wa zamani na afisa wa kijasusi aliyekuwa karibu na mrithi wa kiti cha mfalme, Mohammed Bin Salman.

Mutreb alisikika  akimwambia Khashoggi kwamba atarudi SaudiArabia kisha baadaye kulisikika sauti ya mwili wa mwandishi huyo ukikatwa kwa msumeno.

Maafisa wa Uturuki hawajaeleza ni wapi walizipata rekodi hizo kutoka ndani ya ubalozi mdogo wa Saudia mjini Istanbul.

Khashoggi, aliyekuwa akiliandikia gazeti la The WashingtonPost, aliuawa muda mfupi baada ya kuingia ubalozini humo mjini Istanbul, Uturuki Oktoba 2.

Jumapili, wizara ya mambo ya nje ya Saudia ilikataa shinikizo la Rais Recep Tayyip Erdogan la watuhumiwa wa mauaji ya Khashoggi kushitakiwa nchini Uturuki.

Kwa upande wake Rais wa Marekani Donald Trump amekataa kumlaumu Mwana Mrithi wa Kiti cha Ufalme Mohammed Bin Salman, licha ya kwamba Shirika laUjasusi la Marekani (CIA) kuhitimisha kuwa aliamuru mauaji hayo.

Mauaji hayo yameathiri taswira ya Saudia na mataifa yaMagharibi yakiwamo ya Marekani, Ufaransa na Canada yameweka vikwazo kwa raia 20 wa taifa hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles