31.1 C
Dar es Salaam
Saturday, November 30, 2024

Contact us: [email protected]

Tembo Trust yatoa elimu ya ukatili kwa wanafunzi

JanethMushi, Longido

Shirika la Kijamii la Tembo Trust, limetoa elimu kwa wanafunzi wa kike wa Shule ya Msingi Orbomba ya namna ya kuripoti matukio ya ukatili yanayowakabili katika jamii zao na kuwataka wanafunzi hao kuwa mabalozi wazuri katika kupinga vita dhidi ya ndoa za utotoni na ukeketaji.

Akizungumza juzi katika mafunzo hayo mwezeshaji wa elimu kutoka shirika hilo, Mery Tembo, alisema kwa sasa katika jamii nyingi hususani za kifugaji wamekuwa wakiwakeketa watoto katika umri mdogo hali inayochangia ukatili kwa mtoto wa kike.

Amesema mbali na ukeketaji kumekuwa na tabia ya kuozesha watoto wa kike wakiwa katika umri mdogo hali inayochangia maambukizi ya Virusi vya Ukimwi, hivyo kuwataka wanafunzi hao kuripoti matukio ya ukatili wa kijinsia wanaofanyiwa ili sheria ichukue mkondo wake na kudhibiti vitendo hivyo.

Kwa upande wake mkurugenzi wa shirika hilo Paulina Sumayani, alisema hadi sasa wamefanikiwa kuwaokoa wasichana 14 waliokuwa wafanyiwe ukeketaji na kuwasaidia kupata haki zao za msingi ikiwamo elimu.

Naye mwakilishi wa wanafunzi kutoka katika shule hiyo, Prisila Lazaro, amewaomba wadau wa maendeleo kushirikiana na serikali kutoa elimu kwa jamii hasa juu ya athari za ukeketaji kwa watoto wa kike ili jamii iachane na mila na desturi potofu.

“Tunaomba wadau waendelee kushirikiana naserikali kutoa elimu kwa wazazi na jamii nzima, kuna wakati hatuna amani ya kurejea majumbani shule zinapofungwa, kutokana na baadhi ya wazazi hasa akina baba kulazimisha watoto wa kike waolewe, wasirudi shule,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles