26.1 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Gawio sababu ya mabadiliko uongozi NMB?

Shermarx Ngahemera



MPAKA sasa hakuna aliyetayari kusema kwenye Benki ya NMB sababu za kiongozi wake Mkuu Ineke Bussemaker  kutoka  haraka kwenye Benki hiyo mwezi huu  au kutokana na benki hiyo kukosa mpangilio wa urithi wa madaraka kwenye chombo hicho.

Wengi  wetu kulikosa tabasamu la bashaha la ‘Diana’ kutoka kwa  Ineke Bussemaker.

Kauli ya Bodi ya Wakurugenzi imeshindwa kuwa wazi juu ya asili ya kutoka kwa kiongozi huyo mahiri ambaye amefanya mengi mazuri  kwa benki hiyo na haswa juu ya kutoa taarifa kwa ghafla  na bila sababu ya wazi na hivyo kuleta minong’ono isiyo na ukweli kwa kukosa maelezo na kuwa gumzo kwa sekta nzima.

Kwa macho ya wengi ni kuwa benki hiyo imekuwa ikifanya vizuri sana kwa miaka yote minne aliyokuwapo hapo ila mwaka jana ambapo benki ilipungua faida kwa kiasi kikubwa kutoka shilingi Bilioni 154  mwaka 2016 hadi  Bilioni 95 mwaka 2017 ikiwa ni pungufu ya asilimia 38 ambayo ni kiasi kikubwa  sana lakini kwa mwaka huo ilikuwa hali ya kawaida kwa benki nyingi nchini  zilipata hasara ya ukubwa mbaimbali kutokana na mikopo chechefu (NPL)

Lakini kinachoshangaza  wengi ni kuwa benki zote za maana nchini zinaonekana kufanya mabadiliko ya uongozi wa juu ikiwa ni mkakati wa kujipanga upya kukabiliana na mabdailiko ya hali ya soko iliyotokana na mabenki yenyewe na wateja wao ambao wanaonekana kukwama na Umazoea.

Baada ya Serikali kufanya mabadiliko makubwa ya uongozi  na sera zake za fedha hasa baada ya Gavana wa Benki Kuu Prof Beno Ndulu kuondoka baada ya mkataba  wake kuisha na kuja Prof Florens Luoga kutoka chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwenye Shule Kuu ya Sheria  kupitia Mamlaka ya Mapato (TRA) alikokuwa kama Mwenyekiti wa Bodi.

Ni kawaida wachezaji wakuu wakibadilika na wachezaji wengine lazima wafuate ili kwendana na mahitaji ya nafasi na mahitaji yao muhimu  katika muundo mzima wa mchezo ili kufanya timu.

Hii inatokana na ukweli kuwa Benki zote kubwa za CRDB, NBC na NMB zimefanya mabadiliko ya viongozi wake wakuu kwani CRDB ameingia  Abdulmajid Nsekela  badala ya mkongwe Dk Charles Kimei kung’atuka baada ya utendaji kazi uliotukuka wa miaka zaidi ya miongo miwili. Naye  notisi yake ya kuacha kazi ya mwaka ilikatishwa  na kuwa mwezi mmoja pekee.

Kwenye mwezi Novemba mwaka huu  benki ya NBC ilimthibitisha  Theobald   Sabi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wake baada ya kukaimu kwa  zaidi ya miezi I8.

Awali Dk Kimei alisema anastaafu kazi lakini kwenye ufunguzi wa Tawi la CRDB Chato Rais Magufuli alisema kuwa asiwe mnyonge kwani Taifa litampatia majukumu mengine kwani bado linamhitaji.

Kwa amelezo ya Bodi NMB, Ineke Bussemaker amepewa majukumu mengine makao makuu ya Benki ya RaboBank ya Uholanzi alikotokea na mmiliki  mwenye hisa  nyingi NMB.

Prof Delphus Rwegasira wa Chuo Kikuu Dar es Salaam Shule Kuu ya Biashara na Uchumi anasema kuwa hakuna haja ya kuwa na shauku  kwani kiachotokea ni kitu cha kawaida katika taasisi hizo kwani kama kungekuwa na matatizo ya utendaji yangejionesha kwenye maeneo mengine; na hivyo kutaka ichukuliwe kila benki kwa mambo yake na sio kwa uchumi mzima wan chi.

“CRDB,NMB  na NBC mabadiliko ya viongozi wao yana utofauti wa kihistoria na maudhui na hivyo ichukuliwe kuwa ni kawaida tu na sio athari na haswa ukizingatia ukweli kwamba sehemu zote za sekta hiyo  neema imeanza kuchomoza kwa uhakika na hivyo kufuta dhana ya kuweko matatizo ,’ anasema Prof  Rwegasira

Isitoshe Kauli ya Bodi NMB inasema kuwa ndani ya miaka minne ya utumishi wake Ineke, benki hiyo imeweza kusitawi na kukua kwa hali na mali na kuwa benki yenye faida kubwa kuliko ikiwa na rasilimali  (assets) zaidi ya shilingi trilioni 5.4 na kuifanya kinara nchini.

“Ameendeleza mpango wa kidigitali wa benki hiyo kwa mafanikio makubwa na kutoa huduma ngazi ya daraja la juu kwa viwango vya kimataifa na kuongeza ushiriki wa makundi yote ya jamii (inclusion ) ya Watanzania kwa kiasi kikubwa.”

Kama ilivyo kawaida yake ya utu na kujali maslahi ya wengi Binti Bussemaker anadai kuwa anafurahia mafanikio  yaliyopatikana NMB kwa maana ya kukua kwa benki na mafanikio ya kibiashara yake.

“Nimefarijika na kutukuka kuwa kwa pamoja tumeweza kufanikikisha mengi kwenye miaka hiyo minne ya mafanikio,” anasema Ineke.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles