28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Merkel kukosa ufunguzi mkutano wa G20

 Buenos Aires, Argentina



Viongozi wa nchi 20 zilizoendelea kiuchumi duniani wamekutana leo mjini Buenos Aires, Argentina, katika mkutano wa kilele ambao unatarajiwa kugubikwa na mivutano ya kibiashara, na mzozo mpya kati ya Urusi na Ukraine.

Rais wa Marekani, Donald Trump, ni miongoni mwa viongozi ambao tayari wametua mjini Buenos Aires, baada ya kuahirisha mkutano wake na Rais wa Urusi, Vladimir Putin, kutokana na mzozo mpya kati ya Urusi na Ukraine katika bahari ya Azov.

Uwepo wa Rais Trump, katika mkutano huo unaleta mkanganyiko vichwani mwa watu, kutokana na sera yake ya Marekani kwanza ambayo imeiweka biashara huria duniani katika hali tete.

Huku watu wakiwa na shauku ya mkutano kati ya Trump, na Rais wa China, Xi Jinping, ambao unatazamiwa kutuliza au kuzidisha wasiwasi wa kibiashara.

Nchi hizo zinazoongoza kiuchumi duniani zimekuwa na mvutano na kuwekeana vikwazo vya kiushuru ambavyo vimeathiri sehemu nyingi za dunia.

Trump, kabla ya kuanza safari yake alizungumzia uwezekano wa kupata makubaliano na China, akisisitiza hana haraka yoyote kwa sababu Marekani inanufaika na vikwazo ilivyoiwekea China.

Wakati viongozi wengine tayari wamewasili nchini Argentina, wakiwemo Waziri Mkuu wa Uingereza na Rais wa Ufaransa, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, anaweza kukosa sherehe za ufunguzi wa mkutano huo muhimu, kwa sababu ndege yake Airbus (Konrad Adenauer), ililazimika kukatisha safari hapo jana ikiwa juu ya anga la Uholanzi, na kutua kwenye uwanja wa Cologne na Bonn, baada ya marubani wa ndege hiyo kubaini hitilafu katika mfumo wa mawasiliano.

Hata hivyo, taarifa ya vyombo vya habari nchini Ujerumani, imesema marubani wa ndege hiyo, wamethibitisha hakukuwa na kitisho chochote cha usalama isipokuwa wachunguzi wataangalia pia uwezekano wa sababu za kihalifu katika masaibu yaliyoikumba ndege hiyo.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles