NMB yawanufaisha wafanyabiashara Soko la Magomeni

0
1936

Lulu Ringo, Dar es Salaam

Benki ya NMB tawi la Magomeni, imetoa elimu kwa wafanyabiashara wa Soko la Magomeni Usalama jijini Dar es Salaam, kuhusu umuhimu wa kuwa na akaunti kwa ajili ya kujiwekea akiba itakayowanufaisha wafanyabiashara hao kujikwamua kiuchumi na kuwasaidia katika uendeshaji wa biashara.

Akizungumza leo katika soko hilo, Ofisa Mauzo wa benki hiyo, Cuthbert Zimbwe, amesema benki hiyo ina akaunti nyingi zitakazoweza kuwasaidia wafanyabiasharana hao kujikwamua kiuchumi iwapo watafuata masharti watakayotakiwa kuyafuata.

“NMB ina akaunti nyingi, kuna akaunti ya Fanikiwa, ambayo inahitaji Sh 20,000 ili kuifungua, Chapuchapu Akaunti, ambayo kila mwezi unapata gawio la asilimia tano kulingana na salio ulilonalo katika akaunti yako akaunti hii inahitaji shilingi 10,000 ili uweze kuifungua na Group akaunti ambayo inafunguliwa kwa Sh 30,000 inayochukua watu kuanzia watano, akaunti hii haina makato yoyote na inagawio la asilimia tatu kila mwaka,” amesema Cuthbert.

Aidha Meneja huyo ameweka sawa maana ya dhamana ya mkopo ili kuwatoa hofu wafanyabiashara wenye uoga wa kukopa kutokana na mtazamo wa kuwa dhamana ni fidia ya mkopo wako pale unaposhindwa kulipa mkopo uliokopa.

“Dhamana haina maana ya moja kwa moja kuwa inachukuliwa ili kulipia mkopo wako pale unaposhindwa kulipa, isipokuwa dhamana inakusaidia kufanya kazi kwa juhudi pale unapokumbuka kuweka dhamana kitu chako cha thamani ili kulinda mkopo wako,” amesema Cuthbert.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here