28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Wanaharakati waungana kupinga rushwa ya ngono vyuoni

Kulwa Mzee, Dar es Salaam

Wanaharakati wa Kupinga Rushwa ya Ngono wameunganisha sauti zao na sauti ya Dk. Vicensia Shule, kwa kauli ya vunja ukimya rushwa ya ngono inadhalilisha na kuua.

Akizungumza na waandishi wa habari leo asubuhi hii Mwana Mtandao, Janeth Mawinza, amesema kupitia Dk. Shule amekuwa akidhalilishwa katika mitandao ya kijamii.

“Tunakemea vitendo vya udhalilishaji, usiku Dk. Shule aliandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa ameitwa na kamati ya maadili siku ya leo kuhojiwa kuhusu suala hili.

“Tunakemea kama wanaharakati kuwa vinadhalilisha utu wake na utu wa wanawake wote kwa ujumla,” amesema Janeth.

Akichangia mwanafunzi, Neema Mbise, amesema vitendo hivyo vipo na vinasababisha wanafunzi kufeli na wengine kufaulu kwa sababu ya kukubali kutoa rushwa ya ngono.

“Naishauri Serikali kuweka simu au anuani ya barua pepe (e-mail) ambayo tutafikisha taarifa hizo kwa siri ili kuwakomboa wanawake,” amesema.

Amesema rushwa ya ngono inakwamisha wanafunzi kufikia malengo na wale wanaofikia kama walitoa rushwa ya ngono hawawezi kufanya kazi.

Mwanafunzi wa Chuo cha Utumishi, amesema rushwa ya ngono ifike kikomo inakwamisha juhudi za Serikali kufikia Tanzania ya viwanda kwa kupata watendaji wasioweza kazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles