29.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

China yatoa bilioni 22/- ujenzi vyuo vya ufundi

Na ASHA BANI-DAR ES SALAAM



KATIBU Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dk. Leornad Akwilapo, amesaini mkataba wa kuanza ujenzi wa vyuo vya ufundi stadi vinavyotarajiwa kujengwa nchini na kugharimu Sh bilioni 22.4.

Fedha hizo zimetolewa na Serikali ya China katika kusaidia elimu ya ufundi nchini.

Akizungumza mara baada kutiliana saini ya kuanza ujenzi huo, Dk. Akwilapo alisema lengo ni kuhakikisha vijana wanapata elimu ya ufundi ili kuongeza uchumi.

Alisema nchi inaelekea katika uchumi wa viwanda na Serikali kupitia wizara yake itahakikisha inajenga vyuo vya ufundi nchi nzima kila mkoa.

“Chuo hiki kitakuwa kikubwa na kitakuwa na maeneo maalum ya michezo, sehemu ya chakula na hata nyumba za walimu pia,” alisema.

Pamoja na hali hiyo aliwataka wale wanaosimamia ujenzi wa miradi ya elimu ikiwamo miundombinu  kuhakikisha inakwisha kwa wakati na kwamba hatosita kuwavunjia mkataba watakaoshindwa kufanya hivyo.

Naye mwakilishi kutoka nchini China wa hapa nchini , anayesimamia masuala ya uchumi na biashara, Lin Yuan alisema wameamua kufanya hivyo kutokana na ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na nchi yao huku akiahidi kuendelea kusaidia katika nyanja mbalimbali za kijamii.

Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Pancras Bujulu alisema lengo vyuo viwe nchi nzima ili kuwafanya vijana waweze kuajiriwa na kuwa na uwezo wa kujiajiri.

Alisema wanaishukuru Halmashauri Kagera kusaidia uboreshwaji wa miundombinu kabla ya kuanza kwa ujenzi huo ikiwa ni pamoja na umeme, maji na barabara .

Alisema vyuo vingine vitajengwa Chato, Rukwa, Simiyu, Namtumbo na Kihonda Morogoro.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles