32.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Trump: CIA haijamlaumu bin Salman  mauaji ya Khashoggi

Marekani



Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema Shirika la Kijasusi la nchi hiyo (CIA) halijahitimisha uchunguzi wake kwa kumlaumu mwanamfalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman, kuamuru mauaji ya mwandishi wa habari, Jamal Khashoggi.

Kauli hiyo Rais Trump, ameitoa jana Novemba 22, wakati ambapo Bin Salman, ameanza ziara ya kikazi nje ya nchi yake tangu Khashoggi, alipouawa.

Kwa sasa yupo katika Falme za Kiarabu (UAE) ambayo ni mshirika mkubwa wa Saudia ndani ya kanda ya Mashariki ya Kati.

“CIA wana hisia mbalimbali, ninayo ripoti yao na hawajahitimisha sijui kama kuna mtu ambaye atakuwa na uwezo wa kusema Mwanamfalme Bin Salman, aliamuru mauaji,” amesema Trump.

Taarifa ya maofisa wa CIA kwa vyombo vya habari nchini Marekani, imesema kuwa operesheni ya kumuua Khashoggi, lazima ilihitaji ruhusa ya Bin Salman, ili kutekelezwa.

Huku mamlaka za Saudia zikisisitiza kuwa operesheni hiyo ilikuwa haramu na Bin Salman, hakuwa na ufahamu wowote wa kutokea kwake.

Vile vile, gazeti moja la Uturuki limeripoti kuwa Mkurugenzi wa CIA Gina Haspel, aliwaambia maafisa wa Uturuki kuwa shirika lake lina mkanda wa sauti ya bin Salman akitoa maagizo kuwa Khashoggi anyamazishwe haraka iwezekanavyo.

Wakati huo huo, Ufaransa imetangaza kuwawekea vikwazo raia 18 wa Saudia ambao wanahusishwa na mauaji hayo. Watu hao pia wameshawekewa vikwazo na Marekani, Uingereza na Ujerumani.

Hata hivyo, Bin Salman, hayupo kwenye orodha hiyo, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa amethibitisha.

Khashoggi, aliuawa Oktoba 2, mwaka huu ndani ya Ubalozi mdogo wa Saudia jijini Istanbul, Uturuki. Wakati wa uhai wake alikuwa mkosoaji mkubwa sera za Saudia hususani mwanamfalme bin Salman.

Mwaka 2017, Khashoggi alikimbilia Marekani akihofia usalama wake.

                                                

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles