25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

JK akabidhi vyeti 4,742 UDSM

ANDREW MSECHU NA FERDNANDA MBAMILA


 

RAIS mstaafu Jakaya Kikwete, amekabidhi vyeti kwa wahitimu 4,742 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika awamu ya kwanza ya mahafali ya 48 ya chuo hicho.

Katika mahafali hayo, Kikwete ambaye ni mkuu wa chuo hicho, anatarajiwa kuhitimisha awamu ya pili Jumamosi   ambako atakabidhi vyeti kwa wahitimu  3,072 kutoka Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa.

Akizungumza wakati wa  mahafali hayo jana, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa William Anangisye, alisema chuo hicho kinalazimika kufanya mahafali hayo katika awamu mbili kutokana na kuongezeka   idadi ya wanafunzi, ambao kwa mwaka huu ni 7,814.

Idadi hiyo  ni ongezeko la wanafunzi  725 waliohitimu kutoka idadi ya wanafunzi 7,089 waliohitimu katika mahafali ya 47 yaliyofanyika mwaka jana.

Alisema wanafunzi waliokabidhiwa vyeti vyao jana, 74 walihitimu shahada ya uzamivu, 435 shahada ya Umahiri, 15,Stashahada ya Uzamili, 4137 shahada ya awali, 81 Stashahada na Astashahada.

Alisema miongoni mwa wanafunzi 4,742 waliokabidhiwa vyeti vyao jana, wanawake walikuwa 1,741 au asilimia 36.71.

Alisema katika mahafali ya mwaka huu, katika awamu ya pili ambayo itakuwa na wanafunzi 7814, wanawake watakuwa 2546 au asilimia 32.58.

Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Sakaam, Jaji mstaafu Damian Lubuva alimshukuru Rais Dk.  John Magufuli kwa juhudi zake za kukisaidia chuo na kwa imani  anayoendelea kuonyesha kwa chuo hicho.

Alisema uteuzi anaoufanya rais kwa wahadhiri na wafanyakazi waendeshaji kutoka katika chuo hicho kushika nafasi serikalini   inawapa hamasa ya   kusimamia chuo  kiendelee kutoa elimu bora inayoambatana na maadili mazuri kwa wanafunzi   wawe viongozi bora   baadaye.

Alisema pia anawapongeza wazazi, walezi na wahitimu kwa kufikia hatua hiyo muhimu na kupata tuzo zao kwa kuwa maendeleo ya kweli yanapatikana kwa ushirikiano kati ya Serikali, chuo, wazazi, walezi na jamii.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles