29.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Mawakala 23 mbaroni kwa ‘kuchakachua’ sukari  

Na PASCHAL MALULU



MAWAKALA 23 wa bidhaa za vyakula wakiwamo wafanyakazi wa Mji wa Kahama  wanashikiliwa na polisi wakidaiwa kusamnbaza na kuuaza  bidhaa zinazodaiwa kuchakachuliwa ujazo.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack alisema mawakala hao pia walikutwa wametunza vibaya katika maghala yao bidhaa hizo.

DCaliwaambia waandishi wa habari kuwa  katika ukaguzi   juzi ilibainika mawakala hao wamekuwa wakivujisha ujazo wa bidhaa mbalimbali zikiwamo sukari, chumvi, mafuta ya kupikia na ngano.

Alisema mawakala hao wamekuwa wakipunguza kilogramu 25 hadi 22 na 23  kuwapunja wananchi wakati wa kununua.

Telack alisema  katika baadhi ya maghala ya wafanyabiashara ilikutwa  mifuko   mifuko ya sukari 1000 iliyokuwa haina nembo ya kiwanda chochote.

Alisema mifuko hiyo ikuwa na  nembo za makampuni mengine kama Azania, Kilombero na Kagera Sugar ambayo wamekuwa wakitumia kuhamishia sukari na ngano kutoka nje na kuwauzia wananchi kwa bei tofauti.

“Tumekuta mifuko ya sukari ambayo ina ujazo ambao siyo halali, mfuko wa kilogramu 25 unapunguzwa hadi kilogramu 22.

“Huu ni uhujumu uchumi kwa sababu si ujazo wa kiwandani, tutaendelea na msako huu kila mara na bila taarifa ikiwa ni pamoja na kuwakamata wahusika,” alisema Telack.

Alisema wafanyabiashara hao wote   mashtaka yao yanaandaliwa na watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili ikiwamo kukwepa  kodi kwa kuwa kila wanapopunguza uzito hukwepa kodi ya serikali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles