LAGOS,Nigeria
RAIS Muhammadu Buhari amesema watu wapatao 55 wamepoteza maisha kufutia ghasia zilizozuka katika soko moja lililopo katika Jimbo la Kaduna, Kaskazini mwa Nigeria.
Vifo hivyo vinaripotiwa kutokea baada ya vijana wa Kikristo na Kiislamu wasukuma mikokoteni kuanza kupigana katika soko hilo lililopo katika mji wa Kasuwan Magani.
Kamishna wa Polisi wa Jimbo hilo, alisema kwamba watu zaidi ya 22 wanashikiliwa na jeshi lake na kwamba wameshatangaza hali ya hatari katika mji huo kufuatia machafuko hayo.
“Bila kuwapo uwelewano kati ya makundi tofauti, biashara zetu haziwezi kuendelea,” alisema Rais Buhari.
Alitoa wito kwa viongozi wa jumuiya kuhimiza uvumilivu na kuacha ugomvi huo kabla ya kuendelea na kuwa vurugu.