29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Sirro ataka taarifa sahihi kutekwa kwa Mo, matajiri kutembea na silaha

Bethsheba Wambura, Dar es Salam



Jeshi la Polisi nchini limewataka wananchi kutoa taarifa za kweli zitakazowezesha kupatikana kwa mfanyabiashara Mohammed Dewji maarufu Mo, aliyetekwa Alhamisi wiki iliyopita katika Hoteli ya Colloseum, Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro amesema hayo leo Ijumaa jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hatua jeshi hilo iliyofikia kwenye uchunguzi wa tukio hilo.

Amesema wamekuwa wakipokea taarifa tofauti kutoka kwa wananchi kuhusu alipo Mo ila wakifuatilia wanakuta si za kweli jambo linalosbabisha jeshi kupoteza muda kufuatilia.

“Nawaomba watoa taarifa walete taarifa za usahihi na ukweli, zisiwe na majungu na kuumiza wengine.

“Leo unaambiwa Mo yuko huku unakwenda, unatumia mbwa na askari ukifika huko hayupo, mtu anadhani kwa kubahatisha anaweza akapata zile Sh bilioni moja,” amesema.

Sirro pia amesema jeshi hilo limebaini gari lililotumika kumteka mfanyabiashara Mo, ni Toyota Surf yenye namba za usajili AGX 404 MC rangi ya bluu nyeusi, likiwa linaendeshwa na dereva Zacharia Obasanjo Junior.

Aidha, akizungumzia kuhusu ulinzi, Sirro amesema katika kuhakikisha wanaimarisha ulinzi nchini wamepanga kuleta kamera zitakazorekodi matukio yote katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu, majengo makubwa na katika mipaka yote ya nchi ili kama likitokea jambo lolote inakuwa rahisi kupata kila kilichotokea.

“Mtu yeyote anayetaka kuharibu taswira ya nchi yetu tukimkamata atajua hii ni Tanzania na hata hao waliomteka Mo wajue tukiwapata watatuambia lengo lao kama walitumwa au la, tuwashughulikia kisheria,” amesema Sirro.

Aidha Sirro ametoa rai kwa wananchi kuacha kuhusisha tukio hilo na siasa na wajue kutofautisha kati ya kupotea na kutekwa kwani si kila anayepotea ametekwa ila wengine huamua kuondoka nyumbani na kwenda mbali kutafuta maisha.

“Aidha, tunaendelea kutoa elimu kwa watu waliojaaliwa kuwa na fedha, wasijiachie, watembee na silaha na wasaidizi wao wawe na silaha, pia tusidharau matishio yoyote yanayotokea, tuyaripoti mapema,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles