26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 14, 2024

Contact us: [email protected]

Usingizi hauna adabu, unaweza kukufanya ulale mahali pasipostahili

NANI kasema unahitaji kuwa kitandani tu au mahali popote pale penye staha kama vile kochini chumbani wakati unapohisi umezidiwa na usingizi? Picha hizi hapa chini zinajibu swali hilo kwa vitendo.

Hata hivyo, tukiachana na utani huo, tunaweza kusema ama kweli usingizi hauna adabu!, ni kama vile ambavyo pombe isivyo na adabu kutokana na uwezo wake wa kumuumbua na hata kumshushia mtu hadhi katika jamii mtu ndivyo ambavyo usingizi pia tunatakiwa kuwa makini nao.

Wataalamu wanasema binadamu hutumia theluthi ya maisha yao kwa ajili ya kulala na baadhi hata kwa siku kadhaa, kitu ambacho hata hivyo kwa wengine kinaweza kisitoshe.

Kinaweza kisitoshe kwa sababu mbalimbali kama vile ugonjwa, pombe ama uchovu unaoweza kumfanya mtu afanye lolote popote pale alipo kwa kusinzia bila kujua au kupenda.

Katika suala la uchovu inafahamika wazi wakati mwingine mapambano katika maisha yetu ili mkono uweze kwenda kinywani na hata masomo yenye lengo hilo hilo kwa siku za usoni, humfanya mtu kuwa na shughuli nyingi zinazoweza kumchosha kwa kiwango kikubwa kinachoweza mpoteza umakini au hali ya kujidhibiti.

Watu hawa iwe wakubwa au watoto kutokana na hali hiyo wamejikuta wakisinzia mahala fulani pasipotarajiwa na kugeuka kituko kwa wanaoshuhudia.

Hapa chini tumekuletea picha kadhaa zinazoonesha hali hiyo, kuanzia watoto hadi watu wazima. Watoto wamekutwa wakisinzia juu ya televisheni, katika hafla Ikulu na kadhalika.

Kwa mfano katika suala la Ikulu, hebu fikiria unaposikia umepata fursa ya kwenda kuonana na Rais wa Taifa kubwa kama Marekani na kula naye chakula cha usiku, msisimko wa namna unaupata?

Bila shaka utaifikiria sana, ukiisubiri siku hiyo ifike kwa wingi wa bashasha. Ni wengi hata viongozi wa mataifa mbalimbali duniani wana ndoto ya kuingia White house. Lakini hali kama hiyo ya kimsisimko haikuwa hivyo, kwa mmoja wa watoto waliopata fursa ya kuingia Ikulu.

Mpiga picha wa Ikulu ya Marekani, Pete Souza alichukua kitimbi hicho cha mtoto aliyesinzia wakati ule wa urais wa Barack Obama.

Ilikuwa Juni 14, 2013, Pete alieleza “Rais Obama aliniita ili nimpige picha akipozi na mvulana aliyesinzia katikati ya halfla ya ulaji askrimu wakati wa Siku ya Kina Baba katika chumba cha chakula cha usiku cha White House.”

Picha nyingine tunayoiona hapa chini ni ya mfanyakazi mmoja aliyebambwa na wafanyakazi wenzake akiwa amesinzia mbele ya kompyuta yake kazini. Wafanyakazi hao wa kampuni hiyo ya Reddits wakaamua kupozi nyuma yake huku mwenyewe akiwa hajitambui.

Ni picha ambayo ilitamba sana mitandaoni kiasi kwamba watu wakatengeneza zao na kujipachika wakiwa wamepozi na jamaa huyo, ambaye jina lake halikufhamika mara moja.

Picha nyingine ni ya jamaa aliyekutwa na mkewe akiwa amelala juu ya ng’ombe bada ya kazi ngumu ya kuchunga wanyama hao katika shamba la wanyama huko Wisconsin, Marekani. Ilikuwa ni kitendo rahisi tu cha kwenda ndani ya nyumba kupumzika, lakini mfugaji huyu hakuweza na kujikuta akisinzia ktika mnyama huyo, kitu aambacho kinaweza kuwa hatari kwa maisha yake.

Picha nyingine zikiwamo za kuhatarisga usalama ni pamoja na kulla juu ya tairi la gari lililosimama kwa muda, kulla chooni na kadhalika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles