UN, NEW YORK
BARAZA la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC) limetoa wito wa kusitishwa mara moja mapigano yanayofanywa na makundi yenye silaha katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) ili kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.
Wajumbe wa baraza hilo wamesisitiza kuhusu uharaka wa kuzipeleka timu za madaktari kwenye maeneo yaliyoathiriwa, kwa sababu ugonjwa huo unaweza kusambaa haraka, ikiwemo katika nchi jirani, hali inayoweza ikaathiri utulivu wa kikanda.
Baraza hilo limetoa taarifa hiyo baada ya jana kuarifiwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) katika mkutano mfupi wa faragha uliofanyika kwa njia ya video.
Balozi wa Bolivia Umoja wa Mataifa, Sacha Llorentty Soliz, amesema Ebola na Uchaguzi Mkuu wa Desemba mwaka huu, ni ajenda ya ziara ya maafisa wa baraza hilo nchini Kongo baadae wiki hii.