MAREKANI
Rais Donald Trump ameagiza kuondolewa ulinzi kwa aliyekuwa mkuu wa Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA), John Brennan.
Rais Trump ametoa agizo hilo kwa madai kwamba Brennan ni mtu asiyeeleweka katika uadilifu na asiyefuata misingi.
Brennan alikaririwa akikosoa na kusema mkutano kati ya Rais Trump na Rais Vladimir Putin wa Urusi uliofanyika mwezi July mjini Helsinki, kwamba haukuwa na maana yoyote.
Vilevile aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa hatua hiyo ni jitihada za Rais Trump kudidimiza uhuru wa kujieleza na kuwaandama wakosoaji wa utawala wake.
Brennan amewataka raia wote wa Marekani kutilia mashaka jambo hilo na mwenendo huu wa rais, na kuwatahadharisha wataalamu na wana usalama kuwa makini na hatua hizi za Trump
Kwa upande wake Rais Trump, amekuwa akipuuza madai hayo na kusema kuwa ni jambo linalozushwa tu kwa maslahi ya kisiasa.