A-Z Argentina na Ujerumani
SAOP PAULO, Brazil
FAINALI ya Kombe la Dunia leo jijini Rio De Janeiro ina mvuto wa aina yake. Mechi hiyo itazikutanisha timu za Ujerumani na Argentina zenye kila sifa kutwaa Kombe hilo.
ARGENTINA
Argentina inatarajiwa kumpanga winga wake, Angel di Maria ambaye hayuko fiti kwa asilimia 100. Nyota huyo wa Real Madrid alikosa mchezo wa nusu fainali dhidi ya Uholanzi kutokana na majeraha. Sasa atawapa wakati mgumu mabeki wa Ujerumani.
BAYERN KWA UJERUMANI
Mechi ya nusu fainali dhidi ya Brazil ilishuhudia wachezaji sita wa Bayern Munich wakiwa katika kikosi cha vijana hao wa Kansela Angela Merkel. Bayern Munich imekuwa na mchango mkubwa katika mafanikio ya Ujerumani kupitia kwa Toni Kroos, Manuel Neuer, Jerome Boateng, Bastian Schweinsteger, Philip Lahm, na Thomas Muller.
UBUNIFU
Ujerumani inao viungo wabunifu kama Toni Kroos, Mesut Ozil na Thomas Mueller, ambao wametengeneza nafasi 43 za kufunga kwa pamoja.
MABEKI
Timu zote mbili zilizofika fainali, Argentina na Ujerumani zimekuwa na mabeki imara zaidi ambao wameruhusu mabao matatu langoni mwao. Argentina kuna Pablo Zabaleta, Martin Demichelis na Ezequiel Garay.
Ujerumani kuna Benedikt Howedes, Jerome Boateng, Mats Hummels na Philipp Lahm.