25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 27, 2024

Contact us: [email protected]

Samatta akiri ugumu kwa Msumbiji

Mbwana Samatta
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta

Na Abducado Emmanuel, Dar es Salaam

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta, anayechezea timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, amekiri kuwa mechi ya timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ dhidi ya Msumbiji itakuwa ngumu, kutokana na viwango kushabihiana.

Samatta amepona majeraha yaliyokuwa yakimsumbua ya nyama za paja na sasa yupo nchini Tunisia na kikosi cha Mazembe kinachojiandaa na mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zamalek ya Misri, ambapo anatarajia kurejea nchini kujiunga na Stars kati ya Jumatano au Alhamisi ya wiki ijayo.

Akizungumza kwa mtandao na MTANZANIA Jumapili kutoka jijini Tunis, Samatta alisema ugumu wa mechi hiyo unatokana na upinzani wa baina ya timu hizo, huku pia akidai viwango vinalingana.

“Mechi haitakuwa rahisi kwa sababu hatutofautiani sana viwango vya uchezaji na timu kwa ujumla, vile vile tumekuwa na upinzani, kwani si mara ya kwanza kukutana nao, kwa hiyo lazima ugumu utakuwepo,” alisema Samatta.

Akizungumzia amejiandaaje kukabiliana na Msumbiji, Samatta alisema: “Nafanya mazoezi na timu yangu, tuko katika kipindi cha maandalizi dhidi ya mechi ya Zamalek na mazoezi magumu, nina imani nitakuwa vizuri kwa ajili ya hiyo mechi pia,” alisema.

Stars itavaa na Msumbiji Julai 20 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, katika mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya kuwania kushiriki Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani zitakazofanyika nchini Morocco.

- Advertisement -
Previous article
Next article

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles