Na MWANDISHI WETU – DAR ES SALAAM
POLISI Jamii wawili na dereva mmoja, wakazi wa Mbezi Luis Dar es Salaam, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za uhujumu uchumi kwa kukutwa na meno ya tembo yenye thamani ya Sh milioni 239.5.
Akiwasomea mashataka yaop jana mbele ya Hakimu Mkazi, Ally Salum, Wakili wa Serikali, Faraja Nguka, aliwataja washtakiwa hao kuwa ni dereva mkazi wa Mbezi Luis, Kefas Mlenzi (30), Polisi Jamii, Juma Mtali (35) na Greyson Muhapa maarufu kama Masu (32), wote wakati wa Mbezi Luis.
Wakili Nguka alidai kuwa Juni 28 mwaka huu katika maeneo ya Mbezi Wilaya ya Ubungo washtakiwa kwa pamoja walikamatwa wakiwa na vipande 30 vya meno ya tembo vyenye thamani ya Sh miioni 239.505 bila ya kuwa na kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyama pori.
Washtakiwa hawakuruhusiwa kuzungumza chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kuisikiliza kesi za uhujumu uchumi, isipokuwa mahakama Kuu au kwa kupata kibali kutoka kwa DPP
Kesi iliahirishwa hadi Julai 23, mwaka huu na upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.