32.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

KANSELA MERKEL ATUA MZIGO WA WAKIMBIZI

BONN, UJERUMANI

VYAMA vitatu vinavyounda serikali inayoongozwa na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, vimefikia makubaliano kuhusu sera ya hifadhi kwa wakimbizi, ambayo yametuliza wasiwasi katika kambi ya wahafidhina.

Vyama hivyo vilivyo madarakani, Christian Democratic Union (CDU) cha Bi Merkel, chama ndugu cha Christian Social Union (CSU) cha jimboni Bavaria, na Social Democrats (SPD), vimekubaliana kuharakisha mchakato wa kuwarejesha wakimbizi walioingia Ujerumani wakitokea katika nchi nyingine za Ulaya, ambako walipatiwa vibali vibali vya kuishi.

Kwa mujibu wa makubaliano hayo mapya, hilo litawezekana ikiwa yapo makubaliano baina ya Ujerumani na nchi husika. Hali hiyo inakubaliana na sheria ya sasa ya Umoja wa Ulaya kuhusu hifadhi kwa wakimbizi.

Awali vyama vya kihafidhina vya CDU na CSU vilipata maridhiano ya kujenga vituo vya wakimbizi mipakani, lakini chama cha SPD kilivipinga vituo hivyo, ambavyo vimeondolewa katika makubaliano haya mapya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles