NEW YORK, MAREKANI
STAA maarufu wa mitindo nchini Marekani, Blac Chyna, amejiingiza kwenye uhusiano wa kimapenzi na kijana mwingine mwenye umri chini ya miaka 20 mara baada ya kuachana na YBN Almighty Jay (18).
Mrembo huyo mwenye watoto wawili huku akiwa na umri wa miaka 30, kwa sasa amethibitisha kuwa kwenye uhusiano na Davin Haney mwenye umri wa miaka 19. Kijana huyo amekuwa akijihusisha na mchezo wa ngumi.
Imekuwa ikizoeleka kwa mrembo huyo kujihusisha na watu wa muziki kama ilivyo kwa Tyga ambaye alifanikiwa kupata naye mtoto kabla ya kupata mtoto mwingine akiwa na kaka wa Kim Kardashian, Rob na baadaye kutoka na YBN Almighty Jay ambaye ni msanii wa muziki wa hip hop.
“Davin Haney ni kijana mwenye nguvu, amekuwa kijana wangu na ataendelea kuwa kijana wangu, stori zingine zimepitwa na wakati,” aliandika Blac.