25.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

PROF. KABUDI: UPELELEZI KESI YA UAMSHO KUKAMILIKA PUNDE

Gabriel Mushi, Dodoma

Waziri wa Sheria na Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi amesema upelelezi wa kesi ya Mashekhe wa Jumuiya ya Uamsho Zanzibar, umekaribia kukamilika.

Aidha, amesema Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), inayo mamlaka kisheria kufuta kesi kama ilivyofanya kwenye kesi ya mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline (22).

Akijibu hoja za wabunge waliochangia katika bajeti ya wizara ya Mambo ya Ndani Nchi, bungeni jijini Dodoma leo Mei 4, Profesa Kabudi amesema kesi hiyo imechukua muda mrefu kwa kuwa inahusu suala nyeti la mashtaka ya ugaidi.

Amesema kazi iliyofanyika ni kukusanya ushahidi kutoka ndani na nje ya nchi ambako sasa wizara kwa kushirikia na Ofisi ya DPP inaharakisha kukamilisha upelelezi wa kesi hiyo.

“Jambo hili nataka niwaambie Watanzania kwamba serikali inatambua uwepo wa kesi hii ambayo imechukua muda mrefu mahakamani, nia ya serikali kuona inafikia mwisho, hata hivyo ucheleweshwaji wake unasababishwa na watu wanaojadiliwa na mashataka husika,” amesema.

Pamoja na mambo mengine, amesema DPP anapewa mamlaka na Katiba ya Tanzania Ibara ya 59 na ya Zanzibar Ibara ya 56, hivyo si kweli kwamba amekiuka sheria.

Hata hivyo, amewataka Watanzania kuheshimu jeshi la polisi kwa sababu vyombo vya dola wameapa kufia nchi wakati viongozi wamepa kuilinda katiba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles