24.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 30, 2023

Contact us: [email protected]

WAPINZANI WASUSIA BUNGE WADAI LINAENDESHWA KIBABE

Gabriel Mushi, Dodoma

Wabunge wa upinzani wakiongozwa na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, wametoka ndani ya bunge wakimtuhumu Mwenyekiti wa Bunge Mussa Hassan Zungu, kuliendesha bunge kibabe

Hatua hiyo imekuja baada ya baada ya Lema kuchangia wakati wa kupitisha bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambapo alidai ana jina la Ofisa anayehusika na mauaji.

Baada ya kusema hayo, Zungu alimtajia vifungu vya kanuni za bunge ambapo alimtaka kulifikisha suala hilo kwenye kamati za bunge na litachukuliwa hatua.

Hatua hiyo ilimuibua Zitto ambaye alianza kumtuhumu Zungu analiendesha bunge kibabe ambapo hata alipotakiwa kukaa chini aligoma huku wabunge wengine wakizomea kisha kutoka ndani ya bunge.

Baada ya kutoka nje Lema amezungumza na vyombo vya habari akisema Zungu anaendesha bunge kwa kupendelea upande mmoja huku hoja za wapinzani hazizingatiwi.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,198FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles