24.8 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

FAMILIA YA LISSU YAMSHUKIA SPIKA NDUGAI

Abraham Gwandu, Arusha

Familia ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) imedai kufedheheshwa na kitendo cha Spika wa Bunge Job Ndugai kuingia kwenye mtego wa upotoshaji wa taarifa kwa kudai kuwa Serikali ya Ujerumani ndiyo inayogharamia matibabu Tundu Lissu anayeendelea kutibiwa nchini Ubelgiji.

Akizungumza na waandishi wa habari Jiji Arusha leo Ijumaa Mei 4, msemaji wa familia hiyo wakili Aluthe Mughwai amesema kitendo hicho cha Spika licha ya kuifedhehesha familia yao pia inawavunja moyo wasamaria wema ambao bado walikuwa na nia ya kuendelea kutoa michango yao.

“Nipende kukanusha pia taarifa iliyotolewa wiki mbili zilizopita na mheshimiwa Spika Ndugai kwamba Tundu Lissu matibabu yake yanalipiwa na Serikali ya Ujerumani , sisi familia tulikaa kimya lakini tumeona jambo hili pia tulirekebishe.

“Mimi namuheshimu sana Spika Ndugai ni heri tumkosee mgonjwa au tujikosee wenyewe familia kuliko kumkosea Spika ambaye ni kiongozi mkubwa tusingependa kufika mahali tukalalamika kwamba waandishi wa habari wanaeneza uongo, hata na wewe Spika, hatutaki kufika huko,” amesema.

Hata hivyo, Mughwai amesema habari hizo si sahihi ukweli ni kwamba matibabu ya Lissu yanaendelea kugharamiwa na wasamaria wema walioko ndani ya nchi na nje ya nchi ikiwamo fedha za kujikimu na hii ni pamoja na akiba zake alizonazo yeye na mke wake.

Aidha wakili huyo alisema familia isingeshangazwa na upotoshaji huo kama ungefanywa na watu wengine au vyombo vya habari lakini kitendo cha kusemwa na  kiongozi mkubwa kama Spika ni fedheha isiyoelezeka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,264FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles