27 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

RWANDA YAENDELEA KUWASAKA WATUHUMIWA MAUAJI YA KIMBARI

KAMPALA, UGANDA


RWANDA imewasilisha ombi kwa Uganda, ikitaka kukabidhiwa watuhumiwa 200 wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 wanaoishi hapa ili wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria.

Balozi wa Rwanda nchini hapa, Meja Jenerali Frank Mugambage, aliwasilisha ombi hilo huku akitoa mwito kwa nchi nyingine zenye washukiwa wa mauaji ya kimbari, kusaidia katika kuwakamata ili wafikishwe mbele ya sheria.

Akiongoza  maadhimisho ya mauaji hayo nchini hapa mwishoni mwa wiki iliyopita, balozi huyo alisema ni hatari kwa washukiwa hao kuendelea kuwa huru kwani wanaweza kusambaza chuki zilezile zinazochochea kasumba za mauaji ya kimbari.

Maadhimisho ya awamu ya 24 ya mauaji hayo kwa upande wa Uganda, yalifanyika katika Kijiji cha Kasensero, mgeni rasmi akiwa balozi huyo.

Amelezea kuwa wamekwisha wasilisha majalada 200 kwa Serikali ya Uganda kusaidia kuwakamata washukiwa walioko hapa na wanasubiri mwitikio wa kusaidia hilo.

Mabaki ya zaidi ya miili 10,000 imezikwa katika makaburi ya halaiki kwenye maeneo matatu nchini Uganda.

Akitaja makaburi ya halaiki yaliyoko Uganda kuwa kielelezo muhimu kwa ulimwengu kufahamu athari za mauaji ya kimbari, balozi huyo amewasilisha shukrani za Serikali yake kwa wanakijiji, hasa wavuvi wa Kasensero kwa kujitolea kuopoa miili ya waathirika na kuizika angalau kwa hadhi iliyostahili.

Mahakama Maalumu ya Kimataifa iliendesha mpango wa kuwakamata, kuwafungulia mashtaka na pia kuwahukumu zaidi ya washukiwa 90 wa mauaji ya kimbari katika mahakama iliyokuwa mjini Arusha, Tanzania kati ya mwaka 1994 na 2014.

Lakini hadi sasa Rwanda ingali inawafuatilia wale ambao inadai hawajafikishwa mbele ya sheria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles