31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

MACRON:  SIKWENDA KUMSHAWISHI TRUMP ABADILI MSIMAMO

PARIS, UFARANSA


RAIS Emmanuel Macron, amemaliza ziara yake nchini Marekani, ambayo anasema haikulenga kumshawishi Rais Donald Trump kubadili mtazamo wake kuhusu kujitoa katika mpango wa awali wa nyuklia wa Iran.

Trump anapinga makubaliano ya kimataifa yaliyofikiwa mwaka 2015 yanayolenga kuidhibiti Iran kuhusu mpango wake wa nyuklia, akisema hayawezi kuishinikiza Iran na kwamba kufikia mwezi ujao atatoa uamuzi wa mwisho.

“Sina taarifa za ndani za uamuzi wa Rais Trump kuhusu mkataba wa nyuklia wa Iran (JCPOA). Lakini nilimsikiliza alichosema kuuhusu. Inaonekana hana nia ya kuutetea mpango huo,” alisema.

Pamoja na kwamba jambo hili ni la muda mrefu kabla ya kufikiwa mwaka 2015 likiihusisha Marekani, ukiangalia mtazamo wake inaonekana hawezi kuunga mkono kuendelea na makubaliano ya JCPOA,” alisema Rais Macron.

Macron amesisitiza hakuwa anajaribu kubadili msimamo wa Rais Trump kama inavyodhaniwa na wengi iwapo amepanga kujitoa katika makubaliano hayo.

Lakini alisema Trump anaonekana atafanya kila linalowezekana kuhakikisha mpango wa nyuklia wa Iran unaendelea kuzuiwa.

“Wajibu wangu, hatua yangu haikuwa kujaribu kumshawishi Trump kujitenga na msimamo wake ama kubadilisha akili yake. Naamini tutakachokuwa tunakifanya ni kujenga mshikamano imara.

“Kwahiyo jambo ninalolifanyia kazi ni kuhamasisha. Najaribu kuhakikisha mkataba huu unakuwa wenye tija katika kukabiliana na kuthibiti shughuli za nyukilia za Iran na kuweka mikakati ya kidplomasia ili kuhakikisha uamuzi wowote utakaochukuliwa na Rais Trump hautuathiri,” alisema.

Kupitia ziara yake hii, Rais Macron ameweza kuimarisha ushirikiano na Trump, ingawa katika maoni yake anaonyesha si kwamba wamekubaliana kila kitu bali kuna mambo ambayo wamekuwa na mtazamo tofauti.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles