25.2 C
Dar es Salaam
Monday, December 2, 2024

Contact us: [email protected]

ZAYN MALIK, GIGI HADID ‘WAMWAGANA’

LONDON, ENGLAND


STAA wa muziki nchini Uingereza, Zain Javadd ‘Zayn Malik’ amethibitisha kuachana na mpenzi wake, Gigi Hadid, baada ya kuwa pamoja kwa zaidi ya miaka miwili.

Zayn Malik, ambaye alipata umaarufu wake kwenye muziki baada ya kufanya vizuri kwenye mashindano ya The X Factor, yaliyofanyika mwaka 2010, aliweza kumteka mwanamitindo hiyo mwenye umri wa miaka 22.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, msanii huyo amesema ni maamuzi magumu aliyoyafanya, hasa kwa mtu ambaye alimpenda na kuishi naye kwa kipindi kirefu.

“Napenda kutumia nafasi hii kuwaambia mashabiki zangu kwamba, wanatakiwa kuheshimu maamuzi yangu, najua nimefanya maamuzi sahihi, lakini ni magumu sana, hasa kwa mtu ambaye umekuwa naye kwa kipindi kirefu.

“Ninaamini nitakuwa katika kipindi kigumu, lakini nitakuja kuzoea na yeye atazoea, kwa sasa atakuwa kama rafiki yangu na nitaendelea kumpenda katika maisha yangu yote,” alisema Zayn Malik.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles