AUNT EZEKIEL ATAJA SABABU YA KUMSHIRIKISHA MTOTO WAKE

0
1655

NA JESSCA NANGAWE


STAA wa filamu za bongo, Aunt Ezekiel, amefunguka na kutaja sababu kubwa ya kumshirikisha mtoto wake, Cookie kwenye filamu yake mpya ya ‘Mama’.

Msanii huyo amesema kuwa, lengo lake kubwa la kumshirikisha mtoto wake huyo ni kwa ajili ya kupata uhalisi wa kile alichokifanya kwenye filamu hiyo.

“Nimemshirikisha mwanangu Cookie kwenye filamu yangu nikiwa na maana nyingi, ukiachilia kumwangalia kipaji chake ambacho siwezi kusema ni uigizaji kama mama yake, lakini nimeona nikicheza naye filamu ya Mama ambayo ndani imebeba uhalisia zaidi, itanifanya nicheze kwa kujiamini zaidi kwa kuwa ni mwanangu,” alisema Aunt.

Aunt amesema filamu hiyo inatarajia kutoka wakati wowote mara baada ya maandalizi ya mwisho kukamilika na anaamini itakubalika na wengi, kwa kuwa ametumia ubunifu wa hali ya juu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here