Na Pendo Fundisha, Mbeya
Rufaa ya kupinga hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya katika kesi iliyokuwa inawakabili Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Nyas, Emmanuel Masonga kuanza kusikilizwa wakati wowote.
Hatu hiyo inakuja baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, kutoa namba ya shauri hilo ambapo mmoja wa mawakili anayewatetea washtakiwa hao, Faraji Mangula amesema Mahakama hiyo imepewa namba 29 ya mwaka 2018 na kinachosubiriwa ni tarahe rasmi ya kuanza kusikilizwa kwa rufaa hiyo.
“Tuna matumaini makubwa na mahakama hii itatoa tarehe ya rufaa haraka iwezekanavyo kama tulivyoomba,” amesema.
Februari 26, mwaka huu Sugu na Masonga walihukumiwa kwenda jela miezi mitano baada Mahakama ya Wilaya iliyoongozwa na Hakimu Mfawidhi, Michael Mteite kuwatia hatiani katika kesi ya kutoa lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli.