NA AMON MTEGA,-SONGEA.
MKUU wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo, amewashauri wazazi kuwaelimisha watoto wao wasijiingize kwenye matendo maovu ambayo yanasababisha Taifa kuingia kwenye viashiria vya uvunjifu wa amani.
Jenerali Mabeyo, alitoa wito huo jana mjini Songea mkoani Ruvuma, wakati akihitimisha tamasha la siku ya kumbukizi ya mashujaa waliyonyongwa kwenye vita vya Majimaji na Wajerumani  mwaka 1906 -1907, ambapo mashujaa 67 walinyongwa hadharani wakitetea nchi yao.
Alisema  hivi sasa kumekuwapo baadhi ya vijana wanaojiingiza kwenye vitendo viovu kulingana na utandawazi wa kidunia kinyume na mila na desturi za makabila yao.
Alisema ili kukabiliana na hali hiyo, wazazi wanatakiwa kuendelea kuwaelimisha namna ya umhimu wa kulinda amani kwa kuwa wazalendo kama walivyofanya mashujaa waliopigana vita hiyo.
Inaendelea…………… pata nakala yako ya gazeti la #MTANZANIA