27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 16, 2024

Contact us: [email protected]

SERIKALI,WASHIRIKA WAWEKA MIKAKATI

NA BENNY MWAIPAJA, WFM DODOMA

SERIKALI, imekubaliana na washirika wa maendeleo kurejesha uhusiano wa karibu na wenye tija ili kusaidia kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa miaka mitano na Mkakati wa Kukuza Uchumi Zanziba (MKUZA III).

Hayo yamesemwa mjini Dodoma jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James, wakati akifungua mkutano wa mazungumzo ya kimkakati kama ilivyobainishwa kwenye mwongozo wa ushirikiano wa maendeleo kati ya Serikali na washirika wa maendeleo.

Alisema mwongozo huo wa miaka saba, kuanzia mwaka wa fedha 2017/18 hadi 2014/25, umelenga kuipa Serikali nafasi ya kuongoza mchakato wa maendeleo na kuijengea uwezo wa kukusanya mapato yake ya ndani, kuchambua fursa muhimu za uwekezaji na kutumia masoko ya kikanda na kimataifa kupata faida.

“Tumekubaliana  tusimamie mchakato mzima wa maendeleo wenyewe kama nchi, matumizi mazuri ya rasilimali, kuimarisha uwajibikaji, kukuza biashara na uwekezaji wa ndani na nje,” alisema James.

Alisema nchi inajivunia hatua kubwa iliyofikiwa kiuchumi na kijamii,ikiwamo kutambuliwa kimataifa kuwa kinara wa masuala ya ukuaji wa uchumi wa Taifa na uchumi jumuishi.

 

Inaendelea…………. Jipatie nakala yako ya gazeti la #MTANZANIA

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles