23.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

CHANJO SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI YAONYESHA MAFANIKIO

NA VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM

MAJARIBIO ya chanjo  ya saratani ya shingo ya kizazi imeonyesha mafanikio kwa kiwango cha zaidi ya asilimia 70 ambako   wasichana 135,700 katika Mkoa wa Kilimanjaro wamepatiwa chanjo hiyo.

Serikali imesema kutokana na mafanikio hayo, maandalizi ya kuanza awamu ya kwanza ya mpango wa chanjo hiyo kwa wasichana wa umri wa kuanzia miaka 14, yamekamilika.

Zaidi ya Sh milioni 800 zimatarajiwa kutumika katika mpango huo ambao unaotarajiwa kuzinduliwa  rasmi Aprili 25, mwaka huo ukilenga kuwakinga wasichana dhidi ya saratani.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema hayo Dar es Salaam jana   katika kikao cha uhamasishaji na uraghibishaji wa mpango huo kati wizara, viongozi wa dini na wahariri wa vyombo vya habari.

“Dozi hutolewa kwa awamu mbili, katika Mkoa wa Kilimanjaro awamu ya kwanza walipatiwa wasichana 76,000 na awamu ya pili walipatiwa 59,700… katika awamu ya kwanza ya mpango huu tunakusudia kuwafikia wasichana 616,734,” alisema.

Alisema ingawa bado hakuna takwimu zinazojumuisha nchi nzima kubainisha ukubwa wa tatizo hilo, hata hivyo takwimu za Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) zinaonyesha saratani ya shingo ya kizazi ndiyo inaongoza kuwa na wagonjwa wengi.

“Pale ORCI katika mwaka 2016/17 asilimia 32.8 ya wagonjwa waliotibiwa walikuwa ni wa saratani ya shingo ya kizazi na asilimia 12.9 walikuwa ni saratani ya matiti,” alisema.

Alisema asilimia 11.7 walikuwa wa saratani ya ngozi na asilimia 7.6 walikuwa wa saratani ya kichwa na shingo.

Inaendelea…………….. Jipatie nakala ya gazeti la #MTANZANIA

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles